Makala: Wamoto yake Rich Mavoko yatoa ishara ya mapinduzi kwenye muziki wa BongoFlevaMsanii @richmavoko na muasisi wa lebo ya muziki ya BillioneaKid, ameonyesha ari yakurudi rasmi kwe ulingo wa muziki si Tanzania pekee bali Africa kwa ujumla. Mwezi mmoja uliopita aliweza kutoa kibao kipya kwa jina “Bad Boy” alichomshirikisha msanii mwenza na mkongwe kwenye ligi ya soga za usanii wa muziki wa Bongo flava Ambwene Yesaya maarufu kama AY.


Kibao hiki ambacho kimetazamwa zaidi ya mara 500,000 katika mtandao wake wa YouTube kilikua kama kitakasa njia kwani tayari jana mkali huyu wa mavokali chambilecho jina lake Rich Mavoko aliachia kibao kipya kwa jina “Wamoto”.

Wamoto nikibao ambacho kinaongelea mtoto flani hivi muzuri wa umbo, sura na hulka ya kisasa. Ambae anamfanya Rich Mavoko kukosa kabisa usingizi, nakumfanya alazimike kufunguka waziwazi jinsi anavyompenda kupitia kipaji chake cha muziki.

Kuanzia audio kibao hiki ambacho kimetayarishwa na mtayarishaji mahiri wa muziki Africa Moccoh huku akiwa amekitendea haki kwa asilimia 100% kinawaka moto. Upande wa ubora wa video, hapa ndio utamu wa kazi nzima unakolea. Mpangilio mzima wa jinsi Mavoko anavyoingia kwa madaha akiwa kwenye gari la kistaa, rangi zilivyopangwa na kuambatanishwa na maudhui dhabiti ya stori nzima ya wimbo Wamoto ikakoleza utamu ukakolea.

Huyu ndio yule Rich Mavoko ambao wengi wametamani kumuona, yule Rich Mavoko wa Pacha Wangu, akiwa anajisimamia mwenyewe kidede bila ya woga. Mavoko ambae siwatanzania pekee bali Africa nzima, mashabiki wake wamekua na kiu ya kuisikia sauti yake yenye muvuto na uwezo wa kuliwaza wakati anapotoa burudani.

Nahii inaonekana wazi kupitia boksi za maongezi kwenye akaunti zake zote za mitandao ya kijamii na pia chaneli yake ya YouTube jinsi watu wanavyotiririka kwa sifa kedekede salon sifia kwa mioyo yao mikunjufu. Mashabiki wake wanafurahiaNo kumuona amerudi tena.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments