Marioo Amefunguka Kutumia Mamilioni Kufanya VIDEO Akiwa South Afrika

 


Nyota wa muziki wa kizazi kipya, @marioo_tz amesema ametumia Sh milioni 30 kutengeneza nyimbo sita za audio na video zake.


Akizungumza mwishoni mwa wikiendi, #Marioo alisema hiyo ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu kutumia fedha nyingi Ili kutengeneza kazi zenye ubora, ambazo zitawavutia wengi.


"Kwanza nimefanya video sita na audio kibao nimerekodi wakati wa kutoka ukufika watazisikia, na hii video ambayo nimeitoa sasa hivi nimetumia milioni 30 kuishoot kwa hivyo nimefurahi kwasababu ilikua ni ndoto yangu kufanya video nzuri," alisema.


Alisema kazi hizo ikiwemo hiyo video aliyopanga kuachia wakati wowote endapo mambo yatakaa sawa inavionjo tofauti, ambavyo mashabiki wake wote watakuwa na wakati mzuri wa kuburudika.


@marioo_tz nyota anayetamba na nyimbo kadhaa, ikiwemo Inatosha ni miongoni mwa wasanii wanaokuja kwa kasi kwenye soko la muziki huo ambao unazidi kujikusanyia mashabiki wengi.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments