Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mazungumzo ya Libya yamalizika bila kupendekeza serikali ya mpitoPande hasimchini Libya zimekamilisha mazunguzmo ya wiki moja yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa bila ya kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya mpito ambayo ingeongoza nchi hiyo kuelekea uchaguzi mkuu wa Disemba mwaka unaokuja. 
Kaimu mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Stephanie Williams amewaambia waandishi habari mjini Tunis, kuwa mkutano huo uliowakutanisha wajumbe 75 wa Libya haukujadili majina ya watu watakaounda serikali lakini mazungumzo yaliyofanyika yanatia moyo. 
Mazungumzo hayo yalifanyika chini ya shinikizo kali kutoka jumuiya ya kimataifa baada ya Umoja wa Mataifa kufanikiwa kupatikana mkataba wa kusitisha mapigano kati ya pande hasimu nchini Libya mwezi uliopita.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments