Mbowe na Wenzake Waachiwa kwa DhamanaMwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ni kati ya viongozi wa upinzani walioachiwa kwa dhamana leo Jumanne Novemba 3, 2020.


Wengine walioachiwa ni wajumbe wa kamati kuu ya Chadema,   Godbless Lema na Boniface Jacob ambao pamoja na Mbowe walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Novemba 2, 2020 wakiwa kwenye kikao. Zitto alikamatwa leo mchana alipokwenda kuwatembelea kina Mbowe polisi.


Wakili wa Chadema John Mallya amesema viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti polisi Novemba 5, 2020 saa 3 asubuhi.


Mallya amesema viongozi hao wameachiwa baada ya kujidhamini wenyewe na kutakiwa kutotoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha wanaripoti kituoni hapo tarehe waliyopangiwa 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

1 [disqus]:

 1. Inakuwaje..??
  Hawa Mahaini, Wachochezi wanapewa dhamana na kurudi kwenye Kitaa, huku
  mikono yao imeaa Damuza Watanzania..??

  Tumewasikia wakitangaza Hadharani nia
  yao ovu katika kampeni zao Dumavu zisizo kuwa na Sera. Na maJuzi kati
  baada ya matokeo kutangazwa. Macho kumhuzi akatangaza parawanja hatua inayofata. AU MNAWAONEA HAYA MAGAIDI
  HAWA NA GENGEE LAO..??

  Kumbukeni cheche Huzaa Moto.
  Hatulikubai hilo tuko mil 60 na hili
  genge halizidi watu kwa Idadi ya mkono

  SIMU ZA NA KOMPYUTA ZAO NANI ANAZO..?

  KWA HATARI YA USALAMAWAO NA WETU, HAWA NA WENZAO NI WA KUSWEKA NDANI. NA KAWAIDA YA MMOJA WAO HATO RIPOTI ATAJIPELEKA HOSPITALI KAMA KAWA.

  ReplyDelete