Messi kutua Chelsea ?Klabu ya Chelsea imeripotiowa kufuatilia kwa karibu mno hali ya mchezaji Lionel Messi ndani ya Barcelona kama inaweza kumsajili nyota huyo msimu ujao wa majira ya joto.

Lionel Messi to Chelsea? Blues fans spot interesting development on  Instagram

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Hispania, Guillem Balague amedai Chelsea imekuwa ikifuatilia kwa karibu kila kinachoendelea ndani ya Barcelona baina ya Messi na klabu yake.

Muargentina siku za hivi karibuni ameripotiwa kushinikiza kwa uongozi wa Barcelona akihitaji kuondoka jambo ambalo liligonga mwamba, ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Agosti aliwahi kuutumia ujumbe uongozi wake akiweka wazi dhamira yake hiyo ya kutimka.

Hayo yote yalijiri mara baada ya Barcelona kushushiwa gharika ya mabao 8 – 2 dhidi ya Bayern Munich katika hatua ya robo fainali ya Champions League.

Ukiachana na Chelsea klabu ya Manchester City nayo imeonekana ikifukuzia saini ya Messi lakini hata hivyo nyota huyo amewahi kusikika akidai kuwa ataendelea kusalia Barcelona licha ya kutambua hatakuwa na furaha.

Messi mwenye umri wa miaka 33, ameonekana kutokuwa vema msimu huu hasa ukizingatia amefunga jumla ya magoli matatu tu kwenye michezo 10 aliyocheza ligi kuu Hispania La Liga.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments