Mganda Atajwa Kuwa Mbadala wa Fraga Simba
TADEO Lwanga, kiungo anayecheza soka la kulipwa nchini Misri ndani ya Klabu ya Tanta anatajwa kuingia kwenye rada za Simba. Lwanga ambaye ameletwa duniani Mei 21, 1994 ana umri wa miaka 26 ni raia wa Uganda.

 

Kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Tanta alijiunga nayo akitokea Klabu ya Vipers aliyoitumika msimu wa 2017-19 akitokea Klabu ya SC Villa. Mafanikio yake ndani ya SC Villa alicheza jumla ya mechi 50 na kutupia mabao nane.

 

Imeelezwa kuwa Simba ipo katika hesabu za kupata saini ya kiungo mkabaji huyo kama mbadala wa raia wa Brazil Gerson Fraga ambaye yupo nje ya uwanja msimu mzima kwa majeruhi.

 

Fraga alipata majeruhi hayo alipokuwa kwenye majukumu yake ndani ya Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikipambana na Biashara United na ilishinda mabao 4-0.

 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments