Mgogoro wa ukubwa wa kaburi wachelewesha mazishiMazishi yalicheleweshwa kwa muda wa saa mbili baada ya mgogoro wa ukubwa wa kaburi kuibuka katika mazishi ya mzee mwenye miaka 98

Mtoto wa marehemu, Peter Worby alisema baba yake William alitakiwa kuzikwa lakini Padre kutoka kanisa la Old Hall Green huko Hertfordshire alisema kina cha kaburi hilo ni kifupi kuliko inavyostahili hivyo hawezi kuendesha ibada ya maziko hayo

Baada ya kufikiwa kwa makubaliano, kasisi huyo aliruhusu mazishi ya mzee huyo kuendelea, lakini Bwana Worby alisema familia yake ilinyimwa “muda wa kuomboleza”.


Aidha askofu wa Kanisa Katoliki aliomba msamaha kwa kuwaongezea msongo wa mawazo.


Kwa mujibu wa chama kinachoshughulikia masuala ya waliokufa kilisema, hakuna kina maalum ambacho kimepitishwa kisheria lakini Wizara ya Sheria inapendekeza angalau kaburi liwe na kina cha sentimita 61 kuanzia kwenye mchanga wa jeneza linapoishia hadi eneo la juu ya ardhi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE