Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Millioni 103 zilivyotumika kubadili hospitali hii

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURESerikali mkoani Shinyanga  imekamilisha ukarabati wa jengo la watoto wachanga la hospitali ya Mji wa Kahama  lenye thamani ya shilingi millioni 103 pamoja na kuweka vifaa kwa ajili ya kuhudumia watoto njiti na ICU ya  watoto wanaohitaji uangalizi maalum.


Akiongea wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Majengo hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, alisema kuwa ukarabati wa jengo la watoto wachanga umekamilika na  vifaa tayari vimekabidhiwa kwa ajili ya kupangwa  na  kuanza kufanya kazi na kuongeza kuwa  ujenzi wa majengo ya upasuaji uko katika hutua za mwisho kukamilika.
Ufadhili wa fedha za  ukarabati wa jengo hilo umetolewa na Shirika la Kimataifa la Touch Foundation ambalo pia linafadhili ujenzi wa Majengo ya upasuaji katika Hospitali ya wilaya ya Kishapu, Kituo cha Afya Lunguya na Burungwa vyote vya  Halmashauri ya Ushetu na Msalala, wilayani Kahama  Mkoani Shinyanga.Ujenzi wa Jengo la Upasuaji ukiendelea katika hatua za Mwisho jengo hili liko katika Hospitali ya Jakaya Kikwete iliyoko Kishapu Mkoani Shinyanga.


Aidha kwa upande wake Muhandisi wa mkoa wa Shinyanga, Francis Magoti, aliongeza kuwa jengo la watoto wachanga la hospitali ya Mji Kahama hapo awali lilikuwa limechakaa sana, ila baada ya kukarabati na shirika hilo  kumeongeza wodi ya watoto njiti na wodi ya uangalizi maalumu ya watoto wagonjwa (ICU).


Post a Comment

0 Comments