Mnyika adai alichokisema Mdee ni cha uongo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokarsia na Maendeleo, (CHADEMA), John Mnyika, amesema kuwa kitendo cha Halima Mdee, kusema kuwa kitendo cha wao kwenda kula kiapo cha ubunge wa viti maalum kimebarikiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe siyo cha kweli.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 25, 2020, wakati akieleza hatua zilizochukuliwa na chama hicho, kufuatia maamuzi ya wanachama wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee, kula kiapo Bungeni ili hali chama hicho hakikuridhia na wala hakikuwachagua.


"Kauli iliyotolewa jana wakati wa kuapishwa, iliyotaka kujenga ishara kama vile Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe, alihalalisha hili linaloendelea, hiii kauli siyo ya kweli na yeye ndiye atakayeongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama kitakachofanyika Novemba 27, kwa kuwasikiliza wahusika kwanini waliamua kushiriki kwenye huu usaliti na nini kiliwasukuma kufanya hivyo", amesema Mnyika.


Jana mara baada ya kuapishwa Mdee alisema kuwa "Nikishukuru chama changu cha CHADEMA, kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, ambao kupitia wao sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu, viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata".

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ahhhh..!! Myikwa, Muongo na Mzandiki ni wewe na Kibeko alie kiri katika vyombo.

    Kuuwa na Heshima na Adabu ukitaka kuwazungumzia Waheshimiwa Wabunge Wateule. Vinginevyo hatua stahiki dhidi yako itachukuliwa.

    Miitandaoni kutafuta umaarufu muda wake umesha pita. muulize Salumu

    ReplyDelete
  2. Utaitaje Waheshimiwa Wabunge bila kupitia Bunge..??

    Kigaigai na Ndugai wamepelekewa ombi.?

    Msifanye kama mivyo zoea. Hamli chao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadakta Mdau, Amezoea Ruzuku na Ulaji wa Dezo.

      Kina mama Mahiri, Wamejipanga.

      Cheza na Halimaa.?? Salome na kina Ester...huna haya Myika.

      Delete

Top Post Ad