Mo Awachokoza Yanga SC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’, ni kama amepiga kijembe kwa watani wao wa jadi, Yanga, hiyo ni baada ya kutamka kuwa wanatamani kupata upinzani kwenye Ligi Kuu Bara, kauli ambayo inamaanisha kuwa wapinzani wao hao wa jadi wasitegemee kuambulia chochote.

 

Kauli hiyo aliitoa kwenye hafl a fupi na Wabunge ambao ni mashabiki wa Simba iliyofanyika juzi usiku jijini Dodoma iliyokwenda sambamba na utambulisho wa jezi mpya watakazozitumia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mwaka huu.

 

Simba hivi sasa wanapata jeuri ya kutamba kutokana na mataji matatu mfululizo ya ligi kuu waliyoyachukua kwa kuanzia msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2019/20. Mo alisema kuwa ana malengo makubwa na Simba kati ya hayo ni kuijenga Simba ili iwe klabu endelevu hadi vizazi vijavyo kwa kuhakikisha wanafanya usajili wenye tija kwa timu.

 

 

Bilionea huyo alisema kuwa anafahamu kile wanachokihitaji mashabiki wa Simba na kikubwa ni kuona timu inatandaza ‘Pira Biriani’ huku wakipata matokeo mazuri ya ushindi yatakayowapa pointi tatu muhimu ili wautetee ubingwa wao wa ligi.

 

Aliongeza kuwa hakuna kitakachowazuia kubeba ubingwa wa ligi msimu huu, hiyo ni kutokana na ubora wa kikosi chao ambacho kinaundwa na wachezaji wengi wenye sifa na ubora wa kuichezea Simba.

 

“Imefi kia wakati tumekuwa tukitamani kupata upinzani kidogo wa wapinzani wetu kwani tumekuwa tukiongoza hadi inachosha, tunawaomba wapinzani wetu waongeze upinzani ili watupe changamoto.

 

“Nikiwa bado nipo Simba, nimedhamiria kuijenga klabu itakayokuwa endelevu hadi vizazi vijavyo, na hilo linawezekana kwangu, nina malengo makubwa ndani ya Simba. “Na tunadhamiria kujenga klabu iliyo endelevu ili tuendeleze kutandaza Pira Biriani na mwisho wa siku tuwe mabingwa wa ligi, kwani ubingwa maana yake ni Simba na Simba maana yake ni ubingwa,” alisema Dewji.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad