6/06/2022

Mpenzi wa Mbali Ukisema Hakusaliti itakuwa Unajipa Moyo tu

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Naandika haya kwa hisia za maumivu makali sana ila ukweli ni kwamba "Ukiwa na mpenzi wa mbali alafu ukajiaminisha kuwa hakusaliti huko aliko basi utakuwa unajipa moyo tu ila uhalisia siyo huo "


Sijui niseme nina mpenzi au nilikuwa na mpenzi (maana hata haijajulikana tumeachana au bado) ila iko hivi :


Nina mwanamke ambaye alikuwa kama mchumba ingawa hatujatambulishana kwa wazazi bado. Yeye nilimwacha Arusha na mimi nikaja kutafta riziki huku Zanzibar (kuna chaka la ajira nilipata). Hivyo nikawa mbali naye ni kama mwaka na nusu hivi.


Katika kipindi hiki tulichokuwa mbali tulikuwa na panda shuka nyingi sana katika mahusiano yetu (tumeachana na kurudiana kwa vipindi tofauti tofauti).


Mwezi Aprili mwaka huu tuliachana kimwisho mwisho tukakubaliana kila mtu achukue time yake na maisha yake. Kumbe yeye alitamka hivyo kwa hasira tu ila moyoni hakumaanisha.


Kumbe kipindi chote hiki akawa anasubiri nimtafte lakini mimi ‘nimekula buyu’. Akawaagiza watu kadhaa kuja kuniambia kuwa bado ananipenda na hawezi olewa na mwanaume mwingine and son on lakini mimi sikumtafuta wala.


Basi mwezi jana (mwezi Septemba) uvumilivu ulimshinda kanitafta akanambia “mimi bado nakupenda naomba tu turudiane and son on”. Nilimkubalia maana nikikumbuka tushapita mapito mengi sana ya panda shuka nikiwa naye.


Sasa picha linaanza juzi kati (siku 3 zilizopita) kuna binamu yangu mmoja hivi yupo huko Chuga alikuwa na shida ya dawa (Maana huyu dada anauza duka la dawa alisomeaga nursing). Ikabidi amcheki shemeji yake kuwa ana shida na dawa fulani. Akamwambia hapa dukani kwangu hamna ila njoo nije nikupeleke mahali ninaponunuaga kwenye maduka ya jumla.


Binamu akaenda kamfata na boda hadi kwake wakaenda huko kwenye maduka ya jumla. Kwa mujibu wa binamu anasema walienda kwenye phamarcy moja hivi wakamkuta daktari ambaye alikuwa mshikaji halafu huyo daktari kamwambia mpenzi wangu “hizo dawa hazipo hapa mpaka nyumbani”


Cha kushangaza ni kwamba huyo daktari alimpa mpenzi wangu funguo wakaondoka na bro hadi nyumbani kwa daktari kuchukua dawa na walipofika anadai mpenzi wangu alionekana kuwa mwenyeji humo ndani (nyumbani kwa daktari) akachukua dawa wakarudisha funguo.


Swali ninalojiuliza ni huyu mpenzi wangu amepajuaje kwa daktari mpaka akampa na funguo akachukue dawa (kitu kinachomaanisha tayari ni mwenyeji hapo) kama hawana mahusiano naye? Maana hawaishi mtaa mmoja, na hawafanyi kazi pamoja!


Nimebaki na maswali mengi sana, kwa mazingira kama hayo yananipa ushahidi kuwa yule daktari atakuwa anamla mpenzi wangu.


Kingine kinachonipa ushahidi zaidi ni kwamba baada ya kuchukua dawa walipomrudishia daktari ule funguo broo anadai daktari alimuuliza "Unanipa funguo kwani leo hulali huku?” Mpenzi wangu akajibu “Hapana leo silali nilimuaga mama kuwa nitarudi mapema”.


Inaniuma sana japo sina ushahidi wa moja kwa moja kuwa analiwa lakini kwa mazingira hayo hata kipofu ataona kuwa hapa naibiwa. Jana nimuuliza kuhusu hilo suala kawa mkali hataki kulizungumzia na anasema niache kusikiliza maneno ya watu.


Imeniuma sana na mpaka sasa nimeshindwa nimuhukumuje maana najikuta nina stress hadi nashindwa kulala wala kula. Narudia tena "Ukiwa na mpenzi wa mbali halafu unasema hakucheat basi utakuwa unajipa moyo tu"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger