Msekwa "Wale 19 sio Wabunge Tena Katiba ya Nchi Inasema Hivyo"
“Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha” Spika mstaafu Msekwa

“Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba” Spika Mstaafu, Msekwa


Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

2 Comments

 1. Tanabahi kwa wote: Wabunge husika ieleweke hhawaja wacha kuwa wanachama.

  Ni wanachama Waandamizi, Halali na walaaa hatujasikia au kuwaona wakiukana Uanachama wao.

  Ni Mizengwe na mkakati wa wahuni ktk chama na Genge la wachache.

  Waheshimiwa Wabunge wako katika mchakato wa kuto likubali hilo la mitandaoni na kuitisha kikao cha kumwachisha M/ kiti Uwenyekiti na kupata Viongozi Wapya...Utenguzi wa Genge ni muendelezo wa kuwadhulumu Wabunge sttahiki zao na Kuminya wigo wa Demokrasia na mfumo Dume kandamizi
  chamani.

  Hawa ni bado wanachama na Wabunge Wawakilishi mpaka 2025.

  ReplyDelete
 2. Mhariri, Kichwa cha Habari hakiendani na Maudhui.. na ukilinganisha na mtiririko wa mazungumzo ya Msekwa.

  Ushabiki si jambo jema.

  ReplyDelete