Mtanzania Aliyefungwa Kenya Kwa Ugaidi AjinyongaRASHID MBERESERO, Mtanzania aliyehukumiwa kifungo cha maisha nchini Kenya baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika shambulio la kigaidi lililotokea katika Chuo Kikuu cha Garissa mwaka 2015, amejinyonga hadi kufa katika Gereza la Kamiti jijini Nairobi alikokuwa akitumikia adhabu yake.

 

Maafisa wa gereza hilo wamesema Mberesero aliyekuwa na umri wa miaka 26, alijiua kwa kujinyonga na blanketi lake katika dirisha la Block H alikokuwa amefungwa, akisubiri kusikilizwa kwa rufaa aliyoikata.

 

Mberesero alihukumiwa Julai 3, 2019 na watuhumiwa wenzake wawili,Hassan Edin na Mohamed Abdi, baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki kwenye shambulio hilo la kigaidi lililotekelezwa na Al Shaabab na kusababisha vifo vya watu 148.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments