11/05/2020

Museveni: Nimevutiwa ni ushindi wa kishindo wa CCM katika majimbo ya Ilemela pamoja na Hai



Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema alikuwa anafuatilia kwa makini uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 28, 2020, huku akipongeza ulivyoisha kwa amani.

Museveni ameyasema hayo leo Novemba 5, 2020, kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais Dkt John Magufuli, ambapo amesema moja ya vitu vilivyomvutiwa ni ushindi wa kishindo wa CCM katika majimbo ya Ilemela pamoja na Hai.


'Nilikuwa nafuatilia uchaguzi kupitia Television nikaona mama mmoja wa Ilemela ameshinda kwa kishindo, mara nikaona tena Hai nako CCM imeshinda, nikasema sasa kazi nzuri imefanywa na CCM'', amesema.


Aidha Museveni ameomba msaada wa Sukari pamoja na chakula kwa Rais Magufuli ili wananchi wake waweze kujikimu.


''Unajua kwetu walilala kidogo ila sasa wameanza kuamka, Rais Magufuli naomba msaada wa sukari, mazao ya viwanda, ndizi, mahindi na vingine kwasababu kwetu kuna upungufu kwenye soko la ndani'', amesema.


Katika Jimbo la Ilemela, alishinda mbunge Angeline Mabula huku katika Jimbo la Hai Saashisa Mafuwe wa CCM, alishinda kwa kupata kura 89,786 huku Mbowe akiambulia kura 27,684.



HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger