Musk apanda hadi nafasi ya pili kwenye orodha ya mabilionea Duniani, ampiku Bill Gates kwa utajiri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mmiliki wa kampuni ya Tesla ya uzalishaji wa magari ya umeme Elon Musk, amempiku mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates na kuingia nafasi ya pili kwenye orodha ya matajiri wakubwa zaidi ulimwenguni. 

Kwa mujibu wa takwimu za mabilionea za Bloomberg, kampuni ya hiyo ya Tesla inayomilikiwa na Musk, imepanda kiwango cha hisa kwa asilimia 6.5 na kufikia dola bilioni 127 na milioni 900 baada ya ongezeko la dola bilioni 7 na milioni 200. 


Musk mwenye umri wa miaka 49, aliweza kuongeza kipato chake kwa dola bilioni 100 na milioni 300 tangu mwanzoni mwa mwaka huu. 


Kipato cha mwanzilishi wa kampuni ya teknolojia ya Microsoft kutoka Marekani Bill Gates, kimefikia dola bilioni 127 na milioni 700.


Mmiliki wa kampuni ya Amazon kutoka Marekani Jeff Bezos naye ameweza kuhifadhi nafasi yake ya kwanza kama tajiri mkubwa zaidi duniani kwa kipato cha dola bilioni 182.


Takwimu za mabilionea za Bloomberg huchapishwa orodha ya matajiri wakubwa zaidi kwa umma kwa kuzingatia milki zao, mapato ya hisa na raslimali zao zenye thamani ya juu. 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad