Mwakilishi mteule ACT-Wazalendo afariki dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MWAKILISHI Mteule wa Pandani kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Abubakar Khamis Bakar (69) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano tarehe 11 Novemba 2020, akiwa nyumbani kwake Mbweni visiwani Unguja, Zanzibar. 

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu wa Idara ya Uenezi, Habari na Mawasiliano kwa Umma, Salim Bimani 



Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Mbweni, Unguja, atasaliwa alasiri katika Msikiti wa Qabus, uliopo Mazizini na kuzikwa Kianga, Wilaya ya Magharibi 'A' alasiri ya leo.


Abubakar Khamis, pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama na mwenyekiti wa kamati ya maadili ya chama cha ACT Wazalendo.


Abubakar Khamis Bakar, aliwahi kuwa mwandishi wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Mjumbe wa zamani wa Baraza Kuu la CUF.


Mbali na hayo aliwahi kuwa ni mjumbe wa zamani wa kamati ya kutafuta mwafaka Zanzibar, mjumbe pia wa zamani wa kamati iliyofanikisha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.


Pia aliwahi kushika nyadhifa ya kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa 2010 - 2015.


Na mpaka mauti yanamfika alikuwa ni mwakilishi mteule wa kuchaguliwa na wananchi katika jimbo la Pandani, Pemba, kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanya Oktoba 27 na 28 mwaka huu.


Abubakar Khamis Bakar, amezaliwa Novemba 02, 1951 na amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Jumatano, Novemba 11, 2020.

 


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu amrehemu,
    Lipumba na Zito Kambwe wako katika mipango ya kuhudhuria mazishi.

    ReplyDelete

Top Post Ad