Mwakinyo anapanda jukwaani usiku wa leo kutetea ubingwa wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 BONDIA Hassan Mwakinyo anapanda jukwaani usiku wa leo kutetea ubingwa wake wa Mabara wa WBF wa uzito wa super welter dhidi ya bondia Jose Carlos Paz wa Argentina.

 Pambano hilo  la raundi 12 limeandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sport chini ya ukurugenzi na mwanzilishi, Kelvin Twissa na kuthibitishwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa ya Tanzania (TPBRC) na WBF.


 Mbali ya pambano hilo, leo pia kutakuwa na mapambano ambapo mengine kwa bondia Hussein Itaba atazichapa na Alex Kabangu wa  DR Congo ambapo  Fatuma Zarika wa Kenya ataonyeshana kazi na  Patience Mastara  wa Zimbabwe katika pambano la ubingwa wa dunia wa uzito wa super bantam wa WBF na Mtanzania Zulfa Macho atazichapa na Alice Mbewe wa Zambia.


Mbali ya TPBRC, rais wa WBF Howard Goldberg atasimia pambano hilo huku mwamuzi maarufu duniani, Edward Marshall atawachezesha mabondia hao ambao wametambiana kila mmoja kushinda pambano hilo.


Akizungumza mara baada ya kupima uzito, Mwakinyo amesema kuwa anatarajia kushinda pambano hilo  katika raundi za mwanzoni na kuwaomba mashabiki kuwahi kuingia.


“Nataka kufanya staili ya mabondia wa zamani kama Mike Tyson ambaye alikuwa anamaliza pambano huku mashabiki wakiwa katika foleni ya kuingia na wengine wakikata tiketi. Nawaomba mashabiki wa ngumi za kulipwa nchini, kuwahi kukata tiketi na kuwahi kuingia ili washuhudie nikiweka historia nyingine,” amesema Mwakinyo.


Mwakinyo amesema kuwa atahakikisha Paz anaachana na mchezo wa ngumi za kulipwa kutokanana kipigo alichumuandalia.


“Ninachoongea ndicho ninakimaanisha, nataka kuonyesha mimi ni bondia wa aina gani katika familia yetu ambayo mchezo wa ngumi na kickboxing ni moja ya shughuli zake, sina mchezo katika pambano hili,” amesema huku akisisitiza kuwa kamwe hata mdharau mpinzani wake.


Paz amesisitiza kuwa mikono yake ndiyo ‘itaongea’ ulingoni katika kuthibitisha ubora wake. “Najua Mwakinyo anaongea sana, ni kawaida, lakini mimi nitaonyesha vitendo na kuondoka na mkanda huu,” amesema Paz kwa kifupi.


Rais wa WBF, Howard Goldberg amesema kuwa  maandalizi ya pambano la jioni hii yamekamilika na endapo Mwakinyo atashinda pambano hilo, atapata nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia dhidi ya bingwa mtetezi, Lasha Gurguliani wa Georgia ndani ya kipindi cha miezi mitatu.


“Napenda kuwashukuru  kampuni ya Jackson Group Sport kwa kuandaa pambano hili na kurejesha thamani ya ngumi za kulipwa nchini.  Hii ni mara yangu ya saba kuja nchini, lakini sijawahi kushuhudia weledi wa aina hii katika kuandaa pambano,” amesema Goldberg.


Mkurugenzi wa kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa amesema kuwa maandalizi yamekamilika na kwa mara ya kwanza Tanzania inawakutanisha mabondia kutoka nchi nyingine tano duniani na kuweka historia.


Twissa amesema tiketi zinaendelea kuuzwa kwa njia ya Nilipe na Selcom kwa Sh 3 Milioni kwa meza ya watu 10 na  Sh150,000 kwa kwa viti vya kawaida.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad