Mwanamuziki Wiz Khalifa Aingia Katika Kumi na Nane za Cardi B...


Siku moja baada ya waandaaji wa tuzo kubwa za #Grammy kutangaza watakaowania tuzo hizo katika vipengele mbalimbali, Hitmaker wa ngoma "Black and Yellow", #WizKhalifa, alichukua muda wake kujadiliana na mashabiki zake kuhusu wasanii waliofanya vizuri kuachwa kwenye Tuzo hizo akiwemo yeye mwenyewe ambapo alitoa lawama zake kwa waandaaji hao kwa kitendo cha kutotambua mchango wake katika muziki kwani hadi hivi sasa hajawahi kushinda tuzo hiyo.

Sasa, katika nia njema tu ya mdau mmoja wa muziki kutaka kutoa maoni yake juu ya uendeshwaji wa tuzo hizo, akajikuta anakuwa chanzo cha kumjaza #WizKhalifa katika 18 za hitmaker wa ngoma iitwayo "WAP' mrembo #CardiB kupitia comment yake iliyosomeka, “Cardi B kushinda tuzo ya Grammy wakati Nicki (Minaj) hana hata moja, ni ushahidi tosha kuwa hawa (waandaaji wa tuzo za Grammy) hawana wanachokijua kuhusu muziki”

#WizKhalifa akamjibu shabiki huyo kwa comment iliyosomeka, “Wasanii wengi wenye vipaji vya asili, wanakumbana na tatizo hilo” jibu lililopokelewa na Bardi gangs kama dongo kwa msanii wao, #CardiB, kuwa yeye hana kipaji cha muziki cha kuzaliwa nacho.

#CardiB hakuwa mbali na simu yake, kwani muda mfupi baadae alituma screenshot za #WizKhalifa za mwaka 2016 ambazo zilikuwa zikimtia moyo kuwa aendelee kupambana, huku akisindikiza picha hizo na ujumbe uliosomeka, “Hawa ni wana katika dm yangu mwaka 2016, wanakupa nguvu na ushirikiano wa kutosha ukiwa unapambana kupata nafasi, ila mambo hubadilika ukishatoboa rasmi” 

Muungwana #WizKhalifa akauzima moto huo kwa kucomment kwenye tweet hiyo ya #CardiB akimwambia kuwa ushauri aliompa wakati ule ulikuwa mzuri na bado ataendelea kumsupport vya kutosha.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments