Mzee Miaka 60 Kortini Akituhumiwa Kubaka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MZEE mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa shehia ya Finya Wilaya ya Wete amefikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba akituhumiwa kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano.

Mzee huyo anayefahamika kwa jina Haroub Abdalla Hamad pia anatuhumiwa kumfanyia udhalilishaji mkubwa wa kijinsia mtoto huyo jambo ambalo ni kosa kisheria

Kesi hiyo ilisomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Wete chini ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Rashid Magendo, kwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Mkoa alikuwa nje ya Mahakama kikazi.

Imedaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka wa Serikali, Mohammed Said Mohammed, kwamba mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe isiyofahamika ya mwezi 10/2020 baina ya saa 6;30 mchana na saa 11;00 jioni huko Bahren Finya.

Alisema kwamba siku ya tukio, bila ya ridhaa yake alimbaka mtoto wa kike mwenye umri wa mitano (jina tunalo) ikiwa ni kinyume na kifungu cha 108 (1) ,(2) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya adhabu namba 6/2018 sheria za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mwendesha mashataka ametaja kosa jingine mbadala (Alternative Count) la udhalilishaji mkubwa wa kijinsia kinyume na kifungu cha 139 (1),(a) ,(2),(b) cha sheria namba 6/2018 sheria za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Mheshimiwa Hakimu shauri hili limekuja kwa ajili ya kutajwa lakini kwa kuwa lilistahili kusikilizwa katika mahakama ya Mkoa, tunaomba upange tarehe nyingine,” alishauri Mohamed.


Hata hivyo, mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za aina hiyo na mtuhumiwa amepelekwa rumande hadi Novemba 12 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa katika mahakama ya Mkoa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad