Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Namuona Mrithi Wa Vanessa Mdee

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
HIVI karibuni tasnia ya Bongo Fleva na mashabiki zake wenye kupenda muziki mzuri, imehuzunika, baada ya mwanamuziki mkubwa na aliyepeperusha vilivyo bendera ya Tanzania kimataifa zaidi Vanessa Hau Mdee ‘V Money’, kutangaza kuachana na muziki.


 


Vanessa ambaye amewika sana na ngoma kali kama Never Ever, No Body Else but Me, Kisela, Cash Madame, Niroge, Siri, Hamjui, Moyo na nyingine nyingi, alitangaza rasmi kuachana na muziki kwa madai kuwa amepitia msongo wa mawazo (depression), kiasi cha kutengwa na mama yake mzazi.


 


Vanessa amefanya vitu vikubwa akiwa ndani ya tasnia ya muziki ikiwemo kuutangaza muziki Bongo kimataifa zaidi kwa kufanya kolabo na wasanii wakali ndani na nje ya Afrika Mashariki.


Mbali na kolabo tu, Vanessa ni msanii mwenye kipaji ambacho ni ngumu kumfananisha na wasanii wanaochipukia katika kiwanda cha Bongo Fleva.


 


Vanessa alijipatia mafanikio makubwa sana kupitia muziki kwani mbali na kupata jina pia anaaminika kuwa na utajiri mkubwa katika akaunti yake.


Ni mtunzi mzuri wa mashairi, kwani ngoma zake zimekuwa zikipita katika mikono yake mwenyewe.


Swali lilikuwepo kwa mashabiki na wadau wa muziki kuwa nani anaweza kuvaa kiatu cha Vanessa kwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa?


 


Lakini kwa sasa namuona mrithi wa Vanessa katika muziki huu wa kizazi kipya kwa upande wa wasanii wa kike, kwani wamekuwa wakioneshana mabavu kweli kweli.


Makala haya yanakuletea wasanii wa kike ambao mmoja wao anaweza kuwa ndiye mrithi wa Vanessa.


 


ZUCHU


Zuhura Othman almaarufu Zuchu ni Second Lady kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ambaye amesajiliwa miezi kadhaa iliyopita chini ya sataa mkubwa wa muziki hapa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.


Zuchu ameonesha uwezo kwa kuachia ngoma kali zilizo ndani ya EP yake ambazo ni Raha, Wana, Ashua, Kwaru, Hakuna kulala, Mauzauza.


Ngoma zilizo nje ya EP ni msanii huyo ambazo zimebamba ni pamoja na Cheche, Litawachoma na sasa anafanya poa na Nobody akiwa na msanii kutokea nchini Nigeria Joe Boy.


Zuchu amejipatia mafanikio makubwa ikiwemo kupata watazamaji wengi kwenye chaneli yake ya YouTube na kubwa zaidi ni nyimbo zake kuingia kwenye orodha ya nyimbo mia moja bora duniani kote.


 


NANDY


Faustina Charles almaarufu Nandy, ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye amekuwa akifanya poa sana.


Nandy amefanikiwa kufikisha muziki wake kimataifa zaidi kwani tayari ameshirikiana na wasanii wa hapa Afrika Mashariki mfano Willy Paul na Sauti Sol kutoka Kenya.


 


Nandy amejitangaza zaidi na ngoma zake kali kama One Day, Kivuruge, Wasikudanganye, Acha Lizame, Kiza Kinene, Njiwa, Aibu, Dozi na sasa anafanya poa na ngoma ya Do Me aliyofanya na mchumba wake William Lymo ‘Billnass’.


 


Nandy ambaye amewahi kupanda jukwaa kubwa la muziki la Tecno On Stage, amekuwa akisifika kama msanii ambaye anapepea vilivyo ndani ya Afrika Mashariki na hata kusifika kuwa na kiwango kikubwa cha utajiri kupitia muziki na biashara zake, ukiniuliza naweza kukuambia kuwa huwenda anaweza kuwa mrithi wa V Money.


 


MAUA SAMA


Sexy Lady, Maua Sama ni zao la Nyumba ya Vipaji (THT) na kipaji kilichokuzwa na mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Hamis Mwinjuma almaarufu Binamu ama Mwana FA.


Maua amekuwa akifanya poa sana katika ngoma zake, kwani ngoma kama Crazy akiwa na Mwana Fa, Mahaba Niuwe, Iokote, Niteke, Main Chick na nyingine kibao ambapo kwa sasa anakimbiza na mkwaju wake wa Kanidance.


 


Maua amekuwa akisifika kama msanii ambaye hana makuu bali kuchapa kazi kwani ameshiriki kolabo na wasanii wakubwa hapa Bongo na akafanya poa, mfano Mwana FA, Dully Sykes, G Nako, Darassa na wengine kibao ambapo kolabo hizo zimezidi kumpandisha juu msanii huyo na kumuweka katika nafasi ya kuwa V Money ajaye.


 


RUBY


Hellen George almaarufu Ruby, ni mwanamuziki mzuri mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni.


Ruby ambaye ametamba na ngoma kama Na Yule, Kelele, Forever, Alele na nyingine kibao, ameonekana kufanya poa sana na kuvutia mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva.


Ruby ameonekana kuwa na kipaji kikali, lakini kitu ambacho kimekuwa kikimuangusha ni kukaa kimya kwa muda mrefu kwenye gemu japo akikomaa lazima atafika levo za V Money.


 


MIMI MARS


Mariane Mdee ‘Mimi Mars’, ni mdogo wa Vanessa Mdee, na amekuwa akifanya poa sana.


Mimi ambaye anatoka katika mikono ya Lebo ya Mdee Music ambayo mmiliki wake ni dada yake Vanessa, amewika na vibao kama Shuga, Dede, Muwa, Marioo na nyingine kibao.


 


Mimi amekuwa akifanya poa, kwani ana elimu ya kutosha na kipaji ndani yake.


Uwezekano wa kufuata nyayo za dada yake ni mkubwa kwa sababu anajua mienendo yote na njia alizopita Vanessa mpaka kutusua.


Mbali na kutoka katika nyumba ya waimbaji, Mimi ana koneksheni kubwa ya kufika levo za Vanessa, kwa sababu hata safari nyingi za dada yake naye pia alikuwemo.

Post a Comment

0 Comments