Ndugai: Nitawalinda Wabunge Viti Maalum CHADEMA
SPIKA wa Bunge la 12, Job Ndugai, amesema, kanuni za Bunge zinamtaka kuwalinda wabunge walio wachache na maslahi yao, hivyo  ameahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote.

 

Ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiana na TBC aridhio.

 

Kuhusu wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ndugai amesema, wameteuliwa kihalali na kama Chadema wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu.

 

Amesema, majina ya Wabunge wa Viti Maalum amepewa na Tume ya Uchaguzi, yeye kazi yake ni kuwaapisha wabunge hao na ameshafanya hivyo.

 

Spika Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, hajakomaa kisiasa na amemtaka akajifunze kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments