NEC: Majina ya Mdee, Wenzake Tuliletewa na Mnyika
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera leo Ijumaa Novemba 27, 2020 amesema katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika alimuandikia barua  Novemba 19, 2020 yenye orodha ya majina ya wanachama wanaopendekezwa kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum  na kwamba tume hiyo ilitumia orodha hiyo kuteua wabunge wa viti hivyo.
NEC imeeleza hayo wakati kikao cha kamati kuu ya Chadema kikifanyika leo jijini Dar es Salaam kuwajadili wanachama wao 19 ambao Novemba 24, 2020 waliapishwa kuwa wabunge wa viti maalum mjini Dodoma  jambo lililopingwa na chama hicho na kueleza kuwa hakikuyapitisha majina yao na kuitaka tume hiyo kusema ukweli.

Baada ya  wanachama hao kuapishwa, Mnyika alifanya mkutano na wanahabari na kueleza kuwa hakuna kikao kilichokaa na kupitisha majina hayo na kuyapeleka NEC lakini leo tume hiyo imemtaja Mnyika kuwa aliwasilisha majina hayo.

Katika taarifa yake kwa umma, Mahera amesema, “ifahamike kwamba katibu mkuu wa Chadema alimuandikia mkurugenzi wa NEC barua yenye kumbukumbu namba C/HQ/ADM/20/TU/05/141 ya  Novemba 19 ambayo iliwasilisha orodha ya majina ya wanachama wanaopendekezwa kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

 1. Asaanteni kwa Taarifa.

  Mimi mwenyewe nilikuwepo na najua hivyo na nilishangaa.. !! na kupata mshtuko nillivyo muona katika vyombo na hata M/kiti analijua na baraka yake

  Mkanganyiko, nilivyo muuliza umekuja baada ya yeye kutaka kujua wanamwachaje.? Na Waheshimiwa wabunge kusema wana Majukumu binafsi na ya wawakilishwaji wao, hapo ndipo akazungumza na Rafiki yake wa nje na yule akamshauri Ajitose nalo, hata kuwasiliana na Mrema alimkataza akamjibu kama hawawezi watakuangalia kwa kidogo kitu.

  Alichofanya, ni kujitoa KIMASOMASO.

  Waheshimiwa Wabunge 19 ni Wabunge halali kwa matakwa yote. Tuwape ushirikiano wetu sisi wanachama wa ndani na Watanzania kwa ujumla wetu.

  Salome, Bulaya, Matiko, Mdee na wenzenu Tuko Pamoja na nimesha mwambia
  Mwinyi ka Akuombeni Radhi na kipi alidanganya Umma kwa Masilahi yake binafsi,

  KINA MAMA MAJASIRI WAJENGA HOJA CHAPENI KAZI TULIJENGE TAIFA LETU.

  HUYU MWACHIENI JAMUHURI NA SISI AKIWEMO BISWALO KUHAKIKISHA HAWACHAFUENI. KAENI NA AMANI KULITUMIKIA TAIFA.

  ROHO YA KOROSHO HAIJENGI MWINYIKA.

  ReplyDelete