Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

"Nilimroga Bosi Wangu, Akiniona Anisahau" - Frans

 

Muimbaji wa nyimbo za Injili Frans Kalitusi amefunguka kusema kitendo cha kuokoka kumemfanya aache mambo ya kuroga na kushinda kuwaangalia wanawake kwani mambo hayo alikuwa anayafanya kabla ya kujikabidhi kwa Yesu.

Akizungumzia hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, amesema kabla ya kuokoka hakuwa kama alivyo sasa, ila baada ya kuokoka anaona anakubalika na jamii inamuelewa kile anachokifanya kwenye kazi ya kutangaza neno la Mungu.

"Kabla ya kuokoka nilikuwa naenda sana kwa waganga kuroga ili mambo yangu yaende au mwanamke akipita mbele yako unamtamani lakini ukiokoka vile vitu vyote vinabadilika na kufuata mfumo wa Mungu na maelekezo ya Biblia" amesema Frans Kalitusi 

Aidha akaongeza kusema "Nilikuwa nafanya kazi kwenye Chuo cha Ufundi, kuna mali zilipotea kwenye mikono yetu mwisho wa siku tukagundulika, wenzangu wakakamatwa na kufukuzwa ila mimi nikaenda kwa Mganga ili nisiwezi kuonekana, boss wangu akiniona akawa anasahau na kumbukumbu zinampotea"

Aidha msanii huyo amesema baada ya hayo akaamua kufuata neema ya Mungu kwa kuokoka kupitia Mchungaji wake ambapo akaanza kumtangaza Yesu kwamba anaweza kwa yale aliyomfanyia.

Mwimbaji huyu anapatiakana facebook kwa jina la Frans Kalitusi na Instagram anaitwa FransKalitusi

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments