Onyo kali latolewa kwa watakaothubutu kung’oa viti na kufanya vurugu kwenye mchezo wa Simba, Yanga leo

 


KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi, Yanga dhidi ya Simba, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, ametoa onyo kali kwa wale watakaothubutu kung’oa viti na kufanya vurugu kwenye mchezo huo.

Msimu wa 2016/17, timu hizo zilicheza ambapo zilitoka sare ya bao 1-1, bao la Yanga lilifungwa na Amisi Tambwe ambapo mashabiki wa Simba walifanya vurugu na kung’oa viti.


Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar, leo Jumamosi.


Msimu wa 2016/17, timu hizo zilipocheza zilitoka sare ya bao 1-1 lakini bao lililofungwa na Amisi Tambwe, lilisababisha mashabiki waliodhaniwa kuwa ni wa Simba (kutokana na rangi ya nguo zao na upande waliokuwa wamekaa) kung'oa viti.


Akizungumza jijini Dar, Kamanda Mambosasa alisema kuwa kwenye mpira wa miguu kuna matokeo matatu hivyo mashabiki wakubaliane na lolote litakalotokea.


“Mpira una matokeo matatu kuna ushindi, kushindwa na kutoa sare na wajiepushe na mihemko ya kishabiki, mara nyingi baada ya kushindwa watu wanahangaika kung’oa viti kwani viti vinakosa gani, leo umeshindwa na kesho utashinda, suala la kuharibu mali na kufanya vurugu ni uchwara kwenye ushabiki, niwaombe wawe watulivu, wanadi timu zao na wajiandae kwa matokeo,” alisema kamanda

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE