Polepole kula kiapo leo, Ndugai kuzingatia hili

 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo saa 10:00 jioni, atawaapisha wabunge wawili wa Bunge hilo walioteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli, mapema jana.

 

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Novemba 30, 2020, na ofisi ya Bunge, ambapo imeeleza kuwa wabunge watakaoapishwa hii leo ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole, na aliyekuwa mbunge wa viti maalum katika Bunge la 11 kupitia chama cha CUF, Riziki Lulida.


Spika Ndugai anawaapisha wabunge hao kwa kuzingatia kanuni za kudumu za Bunge inayoeleza kuwa endapo mbunge atachaguliwa au kuteuliwa kipindi ambacho hakuna mkutano wa Bunge unaoendelea, Spika atamwapisha katika eneo atakalolipanga yeye. 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

 1. Ahhh...!!! Umetisha Mwendo kasi wetu. Hongera sana Polepole
  Hongera Kipenzi chetu JPJM, Kutuletea huyu Kijana wetu Mwenye Heshma na Unyenyekevu ni msikivu mzzuri.

  Kubwa zaidi, ni kwamba anaelewa Dira yako na Wapi Tunaelekea
  Its a WIN WIN NOMINATION.

  Karibu Mh. Polepole Bungeni, tunakuahidi kuwapeni Ushirikiano wetu wote 21 mlioapishwa.

  Jipangeni kulitumikiia taifa kwa maslahi mapana ya wananchi Usiku na Mchana.

  Tumejipanga Inshallah kuwaombea Dua kina Halima na wenzake baada ya Salat Alfajir Pamoja na nyie wawili jumla 21, itakuwa Gaddafi. Bila kummsahau kipenzi cha mioyo yetu JPM.

  Mwenyezi Mungu akujazeni Subira,Hekma na Busara.
  Na Mahasidi, wanao wasakama kina mama Wabunge wateule washindwe na nia zao ovu walegee.

  TANZANIA KWANZA. UZALENDO MBELE . MAMLUKI HAWANA NAFASI.

  ReplyDelete