Polisi Wakiri Kumshikilia Mazrui, Wenzake 32

advertise here

 


Kamishina wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohamed Haji Hassan amethibitisha polisi kumshikiria naibu katibu mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Nassor Ahmed Mazrui na wenzake 32.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Oktoba 31, 2020 kamishna huyo amesema walikamatwa Oktoba 28, 2020 katika hoteli ya Manson mjini Unguja wakiwa na kompyuta mpakato 34, ipad, simu  na nyaraka alizodai kuwa zilikuwa na baadhi ya matokeo, kwamba   walikuwa wakiingilia matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.


Tangu Oktoba28, viongozi wa chama cha ACT waliwaeleza waandishi wa habari kuhusu kutoweka kwa kiongozi huyo huku mwenyekiti wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad akisema hata walipouliza polisi walielezwa kuwa hawajui alipo.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

1 [disqus]:

  1. Mpelekeni Bara na wenzake Segerea.

    Msiwaone muhali hawa waleta rabsha za
    Amani yetu, Si Pemba tu mpaka Unguja.

    ReplyDelete