Pombe Zahatarisha Uhai wa Maradona

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MCHEZAJI  mkongwe wa Argertina, Diego Maradona, ametolewa hospitali siku ya Jumatano, na kuelekea kliniki ya kurekebisha tabia ili kuacha kutegemea pombe, Maradona, aliliongoza taifa lake katika mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 1986.


Mapema mwezi huu alifanikiwa kufanya upasuaji katika ubongo ili kuondoa kuganda kwa damu.

Wakili wake amesema Diego amepitia kipindi kigumu zaidi katika maisha yake na ilikuwa kama miujiza kukuta damu imeganda katika ubongo wake na angeweza hata kupoteza maisha yake.


“Jambo zuri ni kuwa Diego yuko sawa sasa,” alisema wakili wake, Matias Morla, wiki iliyopita.

Maradona alilazwa katika kliniki ya Ipensa huko Buenos Aires, akiwa anasumbuliwa na anaemia (upungufu  wa damu).


Baada ya upasuaji huo madaktari wamemshauri Maradona kuacha matumizi ya pombe ambayo yanaweza kuchukua uhai wake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad