Promota wa Twaha Kiduku asakwa na polisi kisa hiki hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

  


 INAELEZWA promota wa pambano la ngumi za kulipwa kati ya Mtanzania, Twaha Kiduku na Sirimongkhon Lamthuam raia wa Thailand anatafutwa na Polisi wa kituo cha Kilwa Road kufuatia madai ya kutowalipa mabondia fedha zao akiwemo Kiduku na watoa huduma wengine waliokuwepo katika pambano hilo lililochezwa mwezi uliopita.

Katika pambano hilo ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa PTA jijini Dar, Kiduku alifanikiwa kuibuka na ushindi wa TKO ya raundi ya saba ambayo ilitokana na mpinzani wake kudai bega lake kushtuka kutokana na makonde makali ya Kiduku.


Uchunguzi uliofanywa na Championi Ijumaa umebaini kuwa mabondia wote waliocheza kwenye pambano hilo, walikuwa wamelipwa malipo nusu na wengine hawakulipwa kabisa hali iliyosababisha promota huyo kuingia mitini na kila anapopigiwa simu hutoa sababu mpya.


Championi lilifanikiwa kumpata Kiduku ambaye amekiri kutomaliziwa pesa zake hadi na promota huyo na kudai kuwa kila akimpigia simu amekuwa haipokei.


Baadhi ya mabondia waliokiri kumdai promota huyo anayetafutwa na Polisi ni Juma Misumari na kocha wake kutoka Morogoro, Twaha Kiduku, Maono Ally na Jongojongo kutoka Bagamoyo na Alphonce Mchumia Tumbo.


 Bondia wa zamani Chaurembo Palasa ambaye alimdhamini kwa watu waliotoa huduma kwenye pambano hilo, amekiri kutafutwa kwa promota huyo kutokana na kitendo cha kushindwa kulipa watu wanaomdai fedha zao kwa kazi waliyomfanyia.


“Kwanza nilikamatwa kwa sababu yake maana nilimdhamini katika baadhi ya mambo lakini ajabu hadi sasa hajalipa na hapatikani, nilichofanya nimekata RB katika Kituo cha Barabara ya Kilwa na anatafutwa kwa sababu suala hilo wanamdai wapo wengi sana,” amesema Chaurembo.


Alipotafutwa promota huyo kwa njia ya simu hakuweza kupokea licha ya kuita kwa muda mrefu kabla ya kutuma ujumbe wa kumtaka mwandishi ajitambulishe na hata alipofanya hivyo hakuweza kupokea simu yake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad