Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais JPM: Uwaziri Mkuu Hauna Guarantee, Nampa Pole Majaliwa

 


Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa kazi ya Uwaziri Mkuu haina dhamana kwamba kila atakayeteuliwa atakaa kwa miaka 5 kwani anaweza kufanya mabadiliko wakati wowotwa kulingana na utendaji wa mtu husika aliyepo kwenye wadhifa huo.

 

Magufuli amesema hayo leo wakati akimuapisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, na kusema kuwa kuendelea kwake kukaa madarakani kutategemea na utendaji wake kwa kipindi cha pili cha serikali ya awamu ya tano, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, leo Jumatatu, Novemba 16, 2020.

 

“Nawapongeza walioapa leo, Mawaziri wawili na Waziri Mkuu, sikuwa na haraka sana ya kuteua Baraza la Mawaziri, tuna Wabunge zaidi ya 350, na bado kuna nafasi 10 za Mimi kuteua, Wabunge presha mzishushe, kazi mliyoomba ni Ubunge sio Uwaziri.

 

“Nilikuwa naona kwenye TV Watu wakishangalia Majaliwa amepata miaka 5 kana kwamba nimewaambia atakaa miaka 5, wakazi wa Lindi wakawa wanashangilia Kusini tumepata Waziri Mkuu miaka 5, nafasi za Waziri Mkuu hazina ‘guarantee’ itategemea na ‘performance’ yake.

“Waziri Mkuu wa kwanza alikuwa Mwalimu Nyerere, akafuata Kawawa akatumikia miaka 5, Edward Sokoine akatumikia miaka 3, akaja tena Sokoine akatumikia mwaka 1, akaja Sinde Warioba miaka 5, nawatajia hii miaka ili mjue kazi ya Uwaziri Mkuu isivyo tulia.

“Msishangilie tu Waziri Mkuu kuwa amepata miaka mitano tena muombeeni afikishe miaka 10 kama Sumaye maana nafasi ya Waziri Mkuu wengi walioikalia hawakufikisha miaka 10 haina guarantee, mimi nampa pole, anafanya kazi nzuri nampongeza ila akachape kazi.

“Rekodi ya Sumaye itaendelea kuwepo ya kuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10, aliyemkaribia alikuwa Pinda (Mtani wangu) alipiga radi Kikwete akawa haoni kitu, Waziri Mkuu kafanye kazi, na wale mnaompongeza kuwa amepata miaka 5 mingine mnamuonea tu,hakuna guarantee.

“Mpango umesema Mkeo anakupa raha, mwaka huu hakuna cha raha sana, kwasababu hata mimi sipati raha sana kwa mke wangu, mlikuwa mnamuona Makamu wa Rais anazunguka kila siku unafikiri alikuwa anapata raha kwa Mume wake? Lazima tuteseke wananchi wapate raha..

“Waziri Mkuu siku ile niliyoapa alinitumia Meseji kwamba Rais nakupongeza umeapa vizuri, sikumjibu, nilitaka ajue kuwa “sio yeye” ndio maana siku jina linatajwa machozi yanamlengalenga na mimi machozi yalinilenga niljua ‘anastahili’ ila msimpe guarantee.

“Waziri Mkuu nikupongeze sana, mwaka huu ni mgumu zaidi, raha unazompa mke wako zitapungua, Mpango umesema mke wako anakupa raha sana, mwaka huu siyo raha na wewe Prof. mwaka huu siyo raha sana kwa sababu na mimi sipati raha sana kwa mke wangu,” amesema Magufuli.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

1 Comments

  1. tell them papa JPM, what is required is to deliver good jobs to Tanzanians and not 'kupeana raha'.

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)