Rais Magufuli Apendekeza Tena Jina la Waziri Mkuu

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, leo amependekeza jina la Mhe. Kassim Majaliwa, Mbunge wa Ruangwa kuwa Waziri Mkuu.

 

Jina hilo limesomwa hii leo Novemba 12, 2020, Bungeni Dodoma na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, mara baada ya jina hilo kuwasilishwa na mpambe wa Rais.


"Barua hii imetoka kwa Mh. Rais na kuelekezwa kwangu mimi Spika wa Bunge, na imeandikwa kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushika madaraka yake ndani ya siku 14, atamteua mbunge wa kuteuliwa anayetokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi kuwa Waziri Mkuu, kwa kutekeleza matakwa ya katiba nimemteua Mheshimiwa mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa", amesema Spika Ndugai, wakati akisoma barua ya Rais Magufuli.


Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa, "Mh Rais ameleta jina la Kassim Majaliwa, ili uteuzi wake uthibitishwe na Bunge tukufu kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

1 [disqus]: