Rais wa Iran: Sitojali ni nani atashinda katika uchaguzi Marekani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa sio muhimu ni nani atakayeshinda uchaguzi wa urais wa Marekani na kwamba hawafanyi mipango yao wakitegemea suala hilo.

Akizungumza baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika katika mji mkuu wa Tehran, Rouhani amesema kuwa sera na njia itakayofuatwa na serikali mpya ambayo itaingia madarakani nchini Marekani ni muhimu kwao.


"Sio muhimu kwetu ni nani atashinda huko Marekani. Uchaguzi wa mwisho wa Marekani ulikuwa wa mfano katika mambo mengi na sitaki kwenda kina katika maelezo yake. Ikiwa Marekani itaweka vikwazo kando na itakuwa na heshima hali zetu zitabadilika. Kilicho muhimu ni harakati za kanuni, njia na siasa. Hatujali watu na vyama." alisema Rouhani.


Akibainisha kuwa wanataka Marekani itii sheria, irudi kwenye mikataba ya kimataifa na kuheshimu watu wa Iran, Rouhani alisema,


"Tunataka mtu yeyote atakayeshinda nchini Marekani aheshimu badala ya kuweka vikwazo. Tumepanga uchumi wetu bila kujali ni nani atashinda uchaguzi wa Marekani. Tulihesabu kulingana na mauzo ya nje yasiyo ya mafuta na uzalishaji. Ni vizuri sana ikiwa Marekani itajifunza na kugundua kuwa lazima ichukue njia tofauti."

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad