Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Rais wa Zanzibar Amteua Suleiman Ahmed Salum Kuwa Katibu wa RaisRais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Bwana Suleiman Ahmed Salum kuwa Katibu wa Rais.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kabla ya uteuzi huo Bwana Suleiman Ahmed Salum alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.

Uteuzi huo ameufanya Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Rais Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 6(1) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya mwaka 1997, amemteua Bwana Nahaat Mohammed Mahfoudh kuwa Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar.


Uteuzi huo umeanza leo tarehe 04 Novemba, 2020.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments