Rapper wakike toka Marekani Cardi B Atoa POVU "Mimi Ndio Mwanamke wa Mwaka"


Rapper wakike toka Marekani, #CardiB ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja na rapper kutoka kundi la Migos, Offset ametumia ukurasa wake wa #Instagram kuwatolea uvivu wote wanaobeza yeye kutajwa kama Mwanamke bora wa mwaka 2020 na Billboard kutoka na wimbo wake wa “Wap” aliomshirikisha Megan Thee Stallion kushika nafasi ya kwanza kwenye chart hizi kwa wiki 14.


#CardiB alianza kwa kusema, “Habari za asubuhi, ni mimi Card B na ndio mimi ndio mwanamke wa Mwaka”. Hakuishia hapo aliendelea kwa kusema, "Na nyinyi watoto wa mitandaoni mnaosema ‘lakini ana ngoma moja tu!’


"Ndio nina ngoma moja ambayo imeuza zaidi, ngoma ambayo imesikilizwa zaidi, ngoma ambayo inafikia mauzo ya nakala zaidi ya milioni moja mara sita ndani ya miezi mitatu, ngoma ambayo imemfanya bibi yako acheza kwenye video za TikTok!” alimalizia CardiB.


Ikumbukwe, "Wap" pia imeibua aina ya uchezaji ambao umejipatia umaarufu kwenye mtandao wa TikTok na kumpa #CardiB nafasi ya kwanza kwa mara ya nne kwenye Chart za Billboard Hot 100.


#CardiB atakabidhiwa tuzo yake katika shughuli ya mwaka ya Billboard ya wanawake kwenye muziki tarehe 10, mwezi ujao akiungana na mastaa wengine wa kike kama Jennifer Lopez, Dua Lipa na wengine wengi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments