google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html RC asimamisha watumishi 8 mpaka wa Horohoro | UDAKU SPECIAL

RC asimamisha watumishi 8 mpaka wa Horohoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella, amewasimamisha kazi maofisa 8 wa taasisi tatu tofauti, ikiwemo TRA, TBS na idara ya mifugo katika kituo cha forodha kilichopo mpaka wa Horohoro kwa madai ya kujihusisha na rushwa pamoja na kuisababishia serikali hasara.

 

Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwa RC Shigella, kuwa vitendo vya rushwa vimekithiri katika ofisi za watumishi wa serikali katika boda hiyo, na ndipo alipoamua kuunda kamati maalumu ya uchunguzi iliyoanza kazi yake Novemba 18 kwajili ya kuchunguza mwenendo wa watumishi hao.


"Hapa wamegeuza kuwa ni shamba la bibi, hawa wanaenda kwenye taratibu za kiuchunguzi na vyombo vya dola viwachukue wakaanze kutoa maelezo kwanini wasipelekwe mahakamani, na hapa waletwe watumishi wengine tunataka kituo cha Horohoro kiwe cha mfano kwa kuhudumia wateja", amesema RC Shigella.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad