Roma Mkatoliki "Hivi ni PISI Zimekuwa Cheap Au ni Wanaume ?"
Msanii wa muziki wa HipHop Roma Mkatoliki, @roma_zimbabwe ameeleza kuwa anapata hofu sana kwa watoto wanaozaliwa na kulelewa kwa sasa kwa sababu kesho yao ya mahusiano itakuwa na changamoto kubwa kutokana na mapenzi ya siku hizi yamekuwa rahisi.


Akifunguka hilo kupitia post yake aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram na Twitter, #Roma ameandika kuwa.. 


"Napata hofu sana na watoto wetu tunaowazaa na tunaowalea kwa sasa, kesho yao ya mahusiano itakuwa na changamoto kubwa sana, mahusiano au mapenzi yamekuwa rahisi siku hizi, yaani hakuna kutongozana mnajikuta tu mmeshaanza mahusiano".


"Unakuta kwenye party ya mwamba kuna pisi 8 na zote zinajijua zina-date na huyo mwamba halafu fresh tu daah, hivi ni pisi zipo cheap au wanaume tumekuwa cheap" ameongeza.


Una mtazamo gani juu ya hili? Tuambie ______


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments