Ruvu Shooting Wapania Kuendelea Kugawa Dozi 

UONGOZI wa Ruvu Shooting umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mechi zote za ligi na wataendelea kugawa dozi bila kufikiria kwa kuwa wanahitaji pointi tatu.

 

Ruvu Shooting imekuwa na mwendo mzuri kwa msimu wa 2020/21 ambapo imeweza kuwa ndani ya tano bora baada ya kucheza mechi 12.

 

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani na wataendelea kutoa dozi.

 

“Tupo imara na tutaendelea kupambana kwa ajili ya mechi zetu zijazo, malengo yetu ni kupata pointi tatu muhimu hivyo hakuna kingine zaidi tutakachofanya zaidi ya kutoa dozi,” amesema.

 

Imeshinda mechi sita na sare nne huku ikipoteza mechi mbili kibindoni ina pointi 22 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Novemba 29 Uwanja wa Mabatini.

 

Inakutana na Kagera Sugar iliyotoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Biashara United na Ruvu Shooting imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments