Ticker

6/recent/ticker-posts
.

''Samatta Hakupewa Huduma Inayostahili Aston Villa'' - Mark Afunguka

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Shabiki wa kutupwa wa klabu ya soka ya Aston Villa, Bwana Mark amesema Mbwana Ally Samatta alikuwa mchezaji mzuri sana, nao kama mashabiki walimpenda sana.

 

Mark ameyasema hayo kupitia Kipenga ya East Afrika Radio leo tarehe 5/11/2020, alipofanyiwa mahojiano na mwandishi wetu Nasser Kingu, aliyopo kwenye ziara ya kutembelea viwanja mabalimbali vya timu za ligi kuu England.


''Samatta alikuwa mchezaji mzuri sana, mimi kama shabiki wa Aston Villa na wenzangu wengi tulimpenda sana aina ya uchezaji wake, lakini tunaamini alikosa ushirikiano wa kutosha ili aweze kutufungia magoli mengi, tunamuunga mkono huko alipokwenda kwenye timu ya Fenerbahce''alisema Mark


Mbwana Samatta, alicheza kwa muda mfupi wa miezi 8 tu, alifanikiwa kufunga mabao 2, katika mechi 16 aliyocheza, 14 ya ligi kuu, na mechi 2 ya FA, pamoja na yote alifanikiwa kuinusuru timu kushuka daraja.

Post a Comment

0 Comments