Saruji Kupanda Bei…! Kiwanda cha Dangote Chaomba Radhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


UONGOZI wa kiwanda cha Dangote kinachozalisha saruji mkoani Mtwara kilisimamisha uzalishaji kwa takribani wiki mbili ili kusafisha mashine za kiwanda.

Imeelezwa kuwa, hali hiyo ilisababisha wafanyabiashara watumie fursa kupandisha bei za saruji kwa mfuko hali iliyofanya wananchi walalamike. Bei ya saruji ilipanda hadi kufikia Tsh. 35,000 kwa baadhi ya mikoa.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, alitembelea kiwandani hapo ili kujua kinachoendelea. Mwanasheria wa kiwanda hicho, Clagu Chuma, ameomba radhi kwa kutotoa taarifa.

Mwanasheria wa  Dangote mkoani Mtwara, Clara Koshuma, kwa niaba ya uongozi wa kiwanda cha Dangote amesema uzalishaji ulisitishwa tangu Oktoba 24, 2020 ili kupisha matengenezo ya mitambo bila kutoa taarifa ya usitishaji wa uzalishaji lakini hawajapandisha bei ya saruji.

Aidha, amesema kuwa uzalishaji utaanza Jumatano, Novemba 11, 2020 huku akiwaomba viwanda vingine wasipandishe bei ya saruji kwa wananchi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad