"Sasa Young Lunya amevuka mipaka" - Nikki wa Pili

 


Msanii wa HipHop kutoka kampuni ya Weusi Nikki wa Pili amesema rapa Young Lunya ameweza kwenda mbele zaidi na kuvuka mipaka kwa kutumia 'digital platform' kwenye upande wa biashara kwa wasanii wanaochipukia.

 

"Msanii mchanga wa HipHop anapokuwa anaanza inabidi awe na mipaka ya kuvuka mbele mfano Whozu alitumia 'digital platform' kutoka, mpaka sasa Young Lunya ndiyo ameweza kuvuka mipaka kwa kutumia 'digital', ameenda mbele ya kuwaza kurap ili wengine wafikirie zaidi biashara ili waweze kupenya" 


Aidha Nikki wa Pili ameongeza kusema "Rap sio rahisi kuishika, wasanii wengi wa rap hawana uwezo au hawana watu wakuwasogeza mfano Young Lunya ametumia ujanja hata nyimbo zake zimebebwa kutokana na ubunifu wake"


Young Lunya ni msanii anayewakilisha kundi la OMG Tanzania na tayari ameshaachia kazi zake ambazo zimefanya vizuri kama tikisa kichwa, fimbo, moto, na freestyle session 1,2,3.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments