Senzo Atoa Neno Sakata Lake na Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


BAADA ya jana Novemba 11, 2020 mshauri wa klabu ya Yanga, Senzo Mazingisa kuhojiwa na maofisa wa polisi katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa masaa yasiyopungua matatu kisha kuachiwa huru, mtaalamu huyo wa masuala ya uongozi wa soka ametoa neno kwa wadau wa soka.


Senzo kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram (football_Senzo) aliandika maneno haya


“Mpira wa miguu hautalala kamwe, Sijawahi kugundua kuwa kuhama kutoka Simba kwenda Yanga kunanisababishia uhasama mwingi kiasi hiki, sasa ni dhahiri kwamba nimesababisha kuumizwa na chuki katika undugu wa mpira wa miguu wa Tanzania kwa kiwango ambacho watu watahatarisha yote kuchafua jina langu kwa kutaka kulipiza kisasi. Niko salama na mzima, niko nyumbani na ninatarajia kutumika. Asante wananchi wenzangu, tuko pamoja," aliandika Senzo


Taarifa za mitandao mbalimbali zinadai sababu za senzo kuhojiwa ni kuwepo na tuhuma za mawasiliano  yake na aliyekuwa mkurugenzi wa wanachamba kwenye klabu ya Simba, Hashim Mbaga.


Ikumbukwe Senzo aliwahi kuwa mtendaji mkuu wa Simba ambapo alijiuzulu nafasi hiyo na kwenda kuajiriwa na Yanga ambao ni mahasimu wakubwa wa Simba.


 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Hersi Said amejibu kuhusu sakata hilo akiandika kuwa limefikia sehemu ambayo sio utani tena bali uadui akidai utani umeishia uwanjani.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad