Senzo: Hata Mfanye Nini, Yanga Hatutoki Njiani!

 


MSHAURI wa masuala ya mabadiliko wa Yanga, Senzo Mazingisa, ameweka bayana kuwa licha ya yote ambayo yamemkuta ya kuhojiwa polisi, haitakuwa sababu ya kuitoa klabu hiyo kwenye mipango yake ambayo imejiwekea kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Senzo ameongeza kwamba suala hilo haliwezi kuwa kigezo cha kuitoa klabu hiyo katika kile ambacho wamekipanga katika ligi kuu kwa msimu huu. Hivi karibuni Senzo raia wa Afrika Kusini aliitwa kuhojiwa kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar kwa tuhuma za kuihujumu klabu yake ya zamani ya Simba kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

 

Senzo amesema kwamba suala hilo ambalo limetokea kwake ni sehemu ya changamoto za uongozi ambalo haliwatoi kwenye mipango yao.

 

“Lolote linalotokea sasa ni sehemu ya mchezo, hatuwezi kutoa macho yetu kwenye mpira, tunahitaji kuwa makini na kile ambacho tumekipanga.

 

“Tunaenda mbele na mipango yetu tukiacha masuala haya yaendelee, changamoto za namna hii ni sehemu ya kazi za kiongozi wa mpira, tunataka kuonyesha klabu iko vizuri na inaenda mbele,” alimaliza Senzo.

  

Said Ally, Dar es Salaam

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE