11/11/2020

Senzo Mikononi mwa Polisi
ALIYEKUWA  Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Senzo Mbatha,  anashikiliwa na  polisi kwenye kituo cha Oyster Bay ambapo imeelezwa sababu ni kuhusiana na tuhuma za mawasiliano yake na Hashim Mbaga  yanayodhaniwa yalilenga kuihujumu Simba (kupanga matokeo) kwenye michezo kadhaa.Hivi karibuni Mbaga (aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki-Simba) alikamatwa na Polisi kwa tuhuma za kuihujumu Simba.


Katika hali isiyotarajiwa miezi michache iliyopita Senzo aliandika barua ya kujiuzulu  na baadaye siku chache kutimkia kwa watani wa Simba ambao ni Yanga,  anakofanya kazi mpaka sasa

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger