Serikali Kuinua Sekta ya Sanaa-Dkt. Abbasi

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni msemaji mkuu  wa Serikali Dkt.Hassan Abassi leo Novemba 30, 2020, jijini Dar es Salaam, ameanza ziara ya kukutana na wadau wa sanaa kwa kukutana na Wakuu wa Taasisi za Wizara hiyo zinazoratibu masuala ya sanaa nchini.

Dkt. Abbasi ameelekeza taasisi hizo kuwa kiungo kati ya wadau wa sanaa na Serikali na amezitaka ziwe karibu na wadau hao, ziwahudumie kwa karibu na zaidi zibuni mambo mapya ya kuishauri Serikali katika kutekeleza azma ya kuiinua sekta ya sanaa nchini.

“Serikali imeahidi kuinua sekta ya sanaa na dhamira kubwa ipo; ni juu yenu kushirikisha wadau ili kupata mrejesho sekta inataka kufanyiwa nini na Serikali ili ikue; zama za wanatasnia na taasisi za sanaa kuwa mbali na kila mmoja anakwenda na lake zimekwisha,” alisema Dkt. Abbasi.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

  1. Yes, Abbbas, watendaji mnamwelewa kipeni chetu JPM.
    He is a performance driven prezida.

    Jisaidieni Kumsaidia. Kazi Inaendelea Quantam Speed.

    ReplyDelete