Siku moja visa vipya vya corona zaidi ya elfu thelathini

 


Uingereza imerekodi visa vipya 33,470 vya COVID19 siku moja, ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu kuanza kwa mlipuko huo kwa mujibu wa takwimu za Serikali.


Kufuatia ongezeko hilo, maambukizi yamefikia 1,290,195 huku vifo vikiwa 50,928. Uingereza inaongoza kwa vifo katika Umoja wa Ulaya.


Mamlaka zimesema kiwango cha maambukizi kinaongezeka na ni muhimu namba ziwe chini ili kudhibiti janga hilo kusambaa zaidi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE