Simba "Tupo Tayari Kusaka Ushindi Leo


JOHN Bocco nahodha wa timu ya Simba ameweka wazi kwamba leo watapambana ndani ya Uwanja wa Jos kusaka ushindi kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.Simba itashuka uwanjani saa 12:00 jioni kusaka ushindi mbele ya wapinzani wao Plateau United ya Nigeria kisha mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 4-9 Uwanja wa Mkapa Dar.
Bocco amesema kuwa wanatambua msimu uliopita walishindwa kufika mbali kwenye michuano hiyo jambo ambalo linawapa hasira ya kupambana kusaka ushindi.
"Kila kitu kipo sawa tumejipanga na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ili kupata ushindi na matokeo mazuri.
"Wapinzani wetu tunajua kwamba wamejiaandaa nasi pia tumejiandaa kwa ajili ya kutafuta ushindi ndani ya uwanja, kikubwa ni dua pamoja na wachezaji kutimiza majukumu ndani ya uwanja," amesema.
Msimu wa 2019/20 Simba iliishia hatua ya awali baada ya kutolewa na UD Songo ya Msumbiji kwa faida ya bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kupata sare ya bila kufungana na ule wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba kuambulia sare ya kufungana bao 1-1.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments