Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Simba Yaichapa Kagera Sugar

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 

 

BINGWA mtetezi wa ligi kuu ya Vodacom Simba, wamefanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu mbele ya wakata miwa, Kagera Sugar kwa ushindi magoli 2-0 katika mchezo uliofanyika leo Novemba 4, kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

 

Magoli ya wekundu wa msimbazi Simba yamefungwa mwishoni mwa katika kipindi cha kwanza na Nahodha wao John Bocco dakika ya 42 na Said Ndemla dakika ya 45,  hili linakuwa bao la nne kwa Bocco kwenye ligi kuu.

 

Kwa ushindi huu Simba inafikisha pointi 19 na kukwea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kushuka dimbani mara tisa, Yanga wanaongoza msimamo wakiwa na alama 23.


Baada ya mechi ya leo  Simba inajiandaa kwa mchezo ujao ambao watakuwa wageni wa timu ya wananchi Yanga  , kwenye dimba la Mkapa Jumamosi Novemba 7 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments