11/20/2020

Simba Yajibu Hoja za FFC Kuhusu Uwekezaji wa Mo
KLABU ya Simba imetoa maelezo ya awali juu ya uendeshwaji na uwekezaji wa timu kuanzia ilipoanza mchakato huo mpaka walivyofanikiwa kumpata mwekezaji pekee aliyejitokeza na aliyekidhi vigezo vilivyokuwa vimewekwa, ambaye ni Mohamed Dewji

Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FFC) kutoa taarifa jana Novemba 19 kwamba Simba ndio wanaochelewesha kukamilka kwa mchakato wa mabadiliko.

Baadhi ya hoja za Simba kuhusu uwekezaji wa Mo Dewji ni zifuatazo:

> Hapa nchini, taasisi mbalimbali zinaundwa, kusajiliwa na kuendeshwa kwa sheria tofauti kulingana na malengo ya taasisi Simba kwa muundo wake tangu ianzishwe, sio kampuni ya kibiashara. Ni taasisi iliyosajiliwa na Msajili wa Vyama vya Michezo na pia Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA), kama zilivyo klabu zingine nchini Simba Sports Club sio kampuni ya kibiashara, ingawa ina mapato, mali na madeni.

 

>Moja ya madhumuni ya mabadiliko ndani ya Simba ni kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa Klabu ili iendeshwe kibiashara na kisasa zaidi, kama zilivyo klabu kubwa za soka duniani, mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba ulipitisha azimio la kukubali mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu.

 

> Kwa hiyo, kwenye mchakato wa mabadiliko ya Simba, hatua ya kwanza ni kuibadilisha Simba Sports Club, ambayo inashikiliwa na Wadhamini ili kuwa Simba Sports Club Company Limited, ambavyo itamilikiwa na wanahisa, ambao ni wanachama wa klabu ya Simba ambao watakuwa na asilimia 51 na Mwekezaji ambaye atakuwa na asilimia 49.

 

> Mara baada ya wanachama wa Simba kupitisha uamuzi wa kufanya mabadiliko na kuamua Klabu iendeshwe kibiashara, iliundwa Kamati Huru ya Zabuni iliyoendesha mchakato wa kutathimini thamani ya hisa za Klabu na kualika wawekezaji wengine wenye nia ya kuwekeza kwenye klabu wajitokeze.

 

>Kamati ilibainisha kwamba thamani ya asilimia 50 ya Kampuni itakayoundwa kwa pamoja kati ya Mwekezaji na Klabu iwe shilingi Bilioni 20. mwekezaji pekee aliyejitokeza kuonyesha nia na uwezo wa kulipa kiwango hicho alikuwa Bwana Mohammed Dewji, ambaye alishinda zabuni hiyo.

 

>Baada ya serikali kutoa maelekezo mapya kwamba Mwekezaji apewe asilimia 49, makubaliano (MoU) kati ya Klabu na Mwekezaji yakawa kwamba Mwekezaji atatoa bilioni 19.6 baada ya mchakato kukamilika. Hata hivyo mwekezaji ameamua atalipa zaidi ya kiwango kilichoainishwa kwenye makubaliano (MoU) ili ifikie bilioni 20, Mkutano Mkuu mwingine wa Wanachama ukaitishwa na kuridhia kwamba Bwana Mohammed Dewji apewe nafasi ya kuwa Mwekezaji.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger