Simon Msuva "Nitakuwa Staa Wydad Casablanca"

 


MCHEZAJI wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva aliyesajiliwa na Wydad Casablanca ya Morocco akitokea Difaa El Jadid, amesema kuwa anaamini anakwenda kuwa staa mkubwa kwenye kikosi hicho kutokana na malengo makubwa aliyojiwekea.

Msuva alisema kuwa anajua kuwa atakutana na changamoto kubwa atakapoanza maisha mapya kwenye klabu hiyo ila ni changamoto ambazo atazivuka na kufanya vizuri kama ilivyo kawaida yake akiwa uwanjani na anaamini atakuwa staa kwenye timu hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu Msuva alisema siyo jambo rahisi kuwa staa kwenye timu kubwa kama Wydad Casablanca lakini kwa jitihada zake anaamini atakuja kuwa mkubwa na kufanya vizuri kwenye timu hiyo kwa sababu ana malengo aliyojiwekea ili kuja kuwa mmoja wa wachezaji mastaa wa timu hiyo.

“Nataka nikawe mchezaji mkubwa pale Wydad, najua siyo jambo rahisi, lakini imani yangu inaniambia kuwa nikiweka jitihada na kuishi kwenye malengo nitafanikiwa. Naamini kwa uwezo wa Mungu nitakuwa mchezaji mkubwa pale,” alisema Msuva.

Msuva alijiunga na Wydad wiki iliyopita kwa mkataba wa miaka minne akitokea Difaa El Jadid, lakini kabla ya hapo aliwahi kukipiga kwenye klabu ya wananchi, Young Africans

GPL

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments