Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Siri ya mdudu 'asiyeweza kufa hata akikanyagwa na gari' yafichuliwa


Maelezo ya picha, Mdudu huyo hawezi kuruka lakini anaweza kujifanya amekufa kujikinga dhidi ya maadui

Mdudu huyu ni mmoja wa viumbe wa ajabu duniani kutokana na maumbile yake ambayo inamwezesha kuponea kifo hata akikanyagwa na gari.


Pengine huenda unajiuliza mdudu huyu ametoa wapi uwezo huo wa ajabu.


Wanasayansi wamekuwa wakichunguza siri ya jinsi mududu huyo anavyoweza kuhumidi uzito wa hadi tani mara 39,000 ya uzaniw a mwili wake.


Na matokeo yanaweza kutoa dalili ya vifaa vikali vya ujenzi kwa matumizi ya ujenzi na anga.

Utafiti huo uliyochapishwa katika jarida Nature, huenda ukatoa mwelekea wa kuunda "vifaa ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuhimili uzito wa aina yoyote", linasema kundi hilo linalo ongozwa na David Kisailus kutoka chuo kikuu cha California, Irvine.


Mdudu huyo wa ajabu anapatikana Marekani na Mexico, ambako wanaishi chini ya magamba ya miti au chini ya miamba. Mdudu huyo ana mifupa migumu zaidi akilinganishwa na wadudu wengine duniani.


Wakusanyaji wadudu wa zamani waligundua hilo walipojaribu kukumdungilia kwenye ubao kwa kutumia pini. Pini zao zilikunjika au kuruka, na walilazimika kutumia kifaa maalum kutoboa mwili wake kutoka upande wa juu.Wadudu hao walipopoteza uwezo wao wa kuruka ili kuepuka hatari, sasa wameguka kiasi cha kuwa mabawa yao ya mbele haiwezi kuvunjika ili kuponea kifo kutokana na kudonwa na ndege wenye njaa.


Exoskeleton cross-section

Maelezo ya picha, Mfuma ya mdudu huyo ana mifupa yenye viungo vya kuingiliana ambavyo hufanya iwe ngumu sana

Watafiti walitumia vifaa maalum vilivyowawezesha kubaini jinsi mifupa ya mdudu huyo ilivyo na viungo vingi vilivyoshikamana ambayo vinaiwezesha kuhimili uzito wa hadi tani 149 (karibu mara 39,000 ya uzito wa mwili wa mdudu huyo).Kufanyia majaribio uwezo wa vifaa hivyo kwa kuunganisha plasitiki na chuma, wanasayansi walitengeza msururu wa viungo kutoka kwa chuma unaolinganishwa kuwa na uwezo kama wa mdudu. Wanasema muundo wa vifaa hivyo umeimarisha uwezo na ugumu wa vifaa vyenyewe


Viungo vingine vya asilia kama vile mifupa, meno na mgamba, vinatumiwa na wanasayansi kama mwongozo wa kuunda vifaa vipya.


Baadhi ya vifaa hivyo vina uwezo mkubwa wa kiufundi pamoja na nguvu, ugumu na uwezo wa kujiponesha.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments