11/09/2020

Somo kwa Mastaa Wanaopenda Kutumia Beat au Midundo ya Wasanii Wengine Bila RuhusaKwa kipindi kirefu sasa imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa wasanii wetu kutumia midundo ya wasanii mbalimbali kutoka nje ya Tanzania kisha kuingiza mashairi yao na kuwa wamiliki wa nyimbo hizo. Inafahamika vizuri kwamba jambo hili ni kinyume na utaratibu wa sheria ya umiliki wa wa kazi za sanaa.

Kugandamizia au ku-sample beat ni kutumia vionjo vya mdundo wa wimbo fulani na kuchanganya kwenye wimbo wako. Kitendo hiki mara nyingi kinafanywa na wasanii wa sasa ambao hutuhumiwa kutumia midundo ya nyimbo za zamani kwa madai kwamba wanatafuta ladha mpya.

Kwa nchini Marekani inapotokea umegandamizia mdundo wa mtu kwenye wimbo wako bila ridhaa yake, kesi yake husababisha mpaka watu kufikishana mahakamani na kulipa fidia si chini ya Dola za Kimarekani laki tano (zaidi ya shilingi Bil. 1.1).

Mfano mzuri ulitokea mwaka 2018 ambapo msanii Meek Mill wa Marekani aliganda mizia beat ya Wimbo wa The Dog Pound Gangstas uliokwenda kwa jina la Big Pimpin kisha kuutumia kwenye wimbo wake wa On Me aliomshirikisha Rapa Cardi B, jambo ambalo wahusika wa wimbo huo hawakupendezwa nalo, lakini msanii huyo aliomba radhi na wakaelewana.

Mwaka huohuo tena, msanii Kojo Funds kutoka nchini Ghana alilipa fidia kisha kuruhusiwa kuendelea na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Check aliomshirikisha mwanadada Raye ambao waliugandamizia kutoka kwenye wimbo wa RnB uliosumbua miaka ya 2000 unaokwenda kwa jina la 7 Day wa Craig David.

Hapa Bongo tumeona matukio kadhaa ya watu kugandamizia beat na kusababisha baadhi ya nyimbo kuzuiwa. Mfano ni Wimbo wa Uno wa Harmonize ambao ulizuiwa na mtayarishaji wa muziki kutoka Kenya anayefahamika kama Magix Enga ambaye alidai msanii huyo aligandamizia beat yake ya Wimbo wa Dundaing.

Kesi nyingine ya kugandamizia beat iliyomkuta msanii Harmonize ni ile ya kufungiwa kwa albam yake nzima ya Afro East ambayo ilitawaliwa na nyimbo ambazo midundo yake imegandamizwa kutoka kwenye nyimbo mbalimbali za zamani kama Fall in Love ambayo imegandamizwa kutoka kwenye wimbo wa msanii 20 Percent aliomshirikisha Bushoke uliokwenda kwa jina la Binti Kimanzi.

Umakini hasa unahitajika kwa wasanii wanapotaka kutumia kazi za watu kwani zinaweza kuwapotezea hadhi ya ubunifu pamoja na kuwa letea gha rama zisizo na msingi ambazo ni hasara kwa upande wa biashara yao ya muziki.

Kuna makubaliano yanatakiwa kufanyika kati ya mmiliki wa kazi ya mwanzo na ambaye anataka kuitumia kwa ajili ya kuongeza ladha kwenye kazi yake ili kuepuka mkanga nyiko mkubwa unao weza kujito keza pale ambapo kazi hiyo itakuwa imetumika bila ridhaa ya mmiliki.

MAKALA: AMMAR MASIMBA

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger